Malezi kwa mtoto ni jukumu la wote

primary school

Shule ya msingi

Shule ya Msingi ya Mt. Placidus, ina Watoto 600, kati ya hao 400 ni wa Bweni. Shule iko umbali wa   Km 6 toka Monasterini. Inapokea Watoto toka Dini zote. Angalia video: #1 e #2

primary school

Shule ya sekondari

Shule ya Sekondari ya Mt. Maurus, ina Wanafunzi 1200. Shule iko umbali wa Km 66 toka Monasterini. Inapokea Wanafunzi toka Dini zote.

Technical school

Shule ya ufundi

Karibu na Monasteri kuna Shule ya Ufundi katika fani ya Umeme, ndogo lakini yenye ufanisi wa juu na inayotambuliwa na wizara ya Elimu Kitaifa. Inapokea Wanafunzi toka Dini zote.

Teacher training college

Chuo cha ualimu

Chuo hiki cha Ualimu kinaandaa Walimu wa Baadaye. Chuo hiki ni kizuri kati ya vyuo vilivyomo ndani ya Mkoa. Kina Wanafunzi 150. Masomo yote yafundishwayo Katika Shule za Monasteri, yanafundishwa na Walimu walio Watawa na wasio Watawa waliopata Mafunzo ya Kudumu ya Ualimu na kujiendeleza katika fani hiyo kwa Maisha yote.

Wamonaki

Wamonaki

Shule ya Wamonaki inapokea na kuandaa Vijana Wakandidati kwa lengo la kuwa Watawa na Mapadre baadaye, katika Malezi Kiutamaduni, Kiroho, Kibinadamu na Kiuchungaji. Angalia video.

Dispensario st. Camilius

Kituo cha afya cha mt. Camilius

Kuna Kituo kwa ajili ya huduma ya Afya, Maabara kwa ajili ya Vipimo, Chumba cha Dawa , Chumba cha Kujifungua.

Farm

Kilimo

Tunalima katika Ardhi ya Monasteri, mazao mbalimbali, kwa ajili ya matumizi ya Jumuiya na kwa wahitaji wetu.

Hospitality

Wageni

Mvimwa tunatoa Mapokezi kwa watu au wageni wanaotaka kututembelea. Tunatangaza Upendo na Tunatoa huduma kwa Wageni kulingana na Kanuni ya Mt. Benedikto RB 53. Tunawahudumia Wageni kwa Unyenyekevu,Upatikanaji na Uwazi kama Ushuhuda wa Upendo na Ukarimu kwa Yesu Kristu, ambaye wageni wetu wanamuwakilisha.

Adoptions

MSAADA KWA WATOTO KUPATA ELIMU

Msaada kwa Mbali Watoto wetu. Shiriki pia wewe pamoja na Kampuni yako, Foundation yako, Taasisi yako, Darasa lako, Familia yako.

Holiday & wedding

Likizo & ndoa

Mapokezi ya Familia Kubwa kwa ajili ya Kuishi katika Utulivu Likizo zako na Fungate yako. Angalia video.